Sunday, 19 January 2020

SIASA MPAKA KWENYE MAKAMPUNI ZA MAWASILIANO, VITAMBULISHO VYA NIDA YAWA GUMZO.

Watanzania wanaendeshwa sana na siasa zisizo kuwa na mipango, wenye siasa yao wameona njia pekee ya kufanya watanzania wajiandikishe ili wapate vitambulisho ni kutoa tamko kuwa kila mtanzania anatakiwa asajili lain yake kwa alama za vidole, mnatishia kufungia watu lain zao bila kusahau hata TCRA haina mamlaka ya kufungia watu mawasiliano ila makapuni ya mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtell, Halotel,  Ttcl...  Ndio yenye uwezo wa kufanya hivyo, pia hiyo inahusu mwenye kampuni yake na wateja wake haihusu wanasiasa hata kidogo. 

1. Uzembe ambo umefanywa na NIDA ndio umesababisha watu mpaka sasa wengine hawana namba za vitambulisho na hata vitambulisho kabisa tena bila haya ukienda kwenye ofisi zao wanakwambia eti namba yako bado endelea kusubiri inakuwaje mnawapa watanzania dead line lakini mnasahau watu wa kupewa dead line ni kina nani,  wanasiasa tumieni akili na sio ndimi zenu. 
2. Makampuni ya mawasiliano hawawezi kupata faida katika biashara zao, makampuni ya simcard zote zitapata hasara maana wanapunguza wateja wao tena kisa siasa mbovu za Tanzania, sasa serikali itailipa makapuni ya mawasiliano ama la? maana mnazisababishia hasara na je mtategemea kulipwa kodi maana mnawapatia hasara za bure. 
3. Makampuni ya mawasiliano mnatakiwa mdai haki yenu, najua mtakuwa na policy zenu na sheria zenu ambazo zinaonyesha nani anauwezo wa kufanya maamuzi katika makamupuni yenu najua hamna sehemu ambayo imeandika mwanasiasa ama raisi wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania. 
4. Watanzania wote mnatakiwa mdai haki yenu ya mawasiliano, mawasiliano ni haki ya kila mtanzania pia hamna serikali bila wananchi, wananchi ndio serikali yenyewe maana nchi bila kodi za wananchi haiwezi kujiendesha pia usisahau katika kulipa kodi mpaka kodi ya mawasiliano unayotumia unalipia. Watanzania tunatakiwa tuache uwoga usio kuwa na maana na kuzidi kuwa watumwa huru katika nchi yetu ambayo ni huru. 
Sasa watanzania dhamana ya mawasiliano yetu ipo katika mikono yetu wenyewe,  ni chaguo letu kuendelea kupelekwa na wanasiasa kama ng'ombe wanaokwenda kunywa maji yaani kukubali kuburutwa na siasa mbovu za Tanzania ama kuamua kudai haki zetu za msingi na kupata kinachostaili katika maisha yetu.