Sifa mojawapo ambayo imetajwa kwa kugombea ambao wanatakiwa kugombea nafasi za watendaji wa mitaa ambayo imetangazwa na serikali ni kuwa na kadi ya uanachama wa chama cha CCM. Leo mapema asubuhi nikiwa katika mahojiano na mwenyenia ya kugombea amesema kwamba ameulizia sifa za kugombea na moja wapo nikuwa lazima awe na kadi ya uanachama wa chama cha CCM.
Tunasema Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi ila ukweli ni kwamba chama kinacho tawala ni kimoja na kinazidi kupoteza maana ya mfumo wa vyama vingi kwa kuwakandamiza wanasiasa wanaotokea kwenye vyama vya upinzani na kuwanyima nafasi ya kuleta maendeleo katika nchi ya Tanzania.
2020 wananchi wote tunatakiwa kuangalia sera ambazo zitasaidia kueta maendeleo katika nchi yetu na si kuchagua chama kama tunavyofanya kwa mazoea ni wakati ambao tunatakiwa kujua kuwa kama kweli miaka 43 ya uongozi wa chama cha mapinduzi CCM mpaka sasa shida ni zilezile tena ndio zinaongezeka kila siku maradufu bora ya jana kwanini tunaendelea kulea siasa ambazo hazina tija nchini mfano marekani wakishida chama cha Republican msimu ujao kinashinda chama kingine ndio maana ata siasa zao zipo viziri maana wananchi wake wanachagua sera na sio chama kama watanzania tunavyofanya.
Kwa wazalendo wote ni vizuri tukapenda nchi yetu na kuchagua sera za maana ambazo zitatuletea mabadiliko chanya nchini.