Vitendo vya kupokea rushwa imeenea/kithiri katika jeshi la polisi sana, inafikipindi mpaka wananchi wanaomba msaada kwa mbunge wao maana wanakuwa wamechoshwa na vitendo hivyo. Katika jimbo moja Tanzania madereva boda boda imewalazimu kuomba msaada kwa mbunge wao ili wanusurike na vitendo vya rushwa kila wakati, nanukuu" mbunge sisi ni madereva bodaboda wa wilaya x(jina la wilaya nalihifadhi) tunaomba msaada wako maana tunanyanyaswa na polisi wa usalama barabarani mpaka tunahofia usalama wetu"
1. Kukamatwa bila sababu ili wapate pesa.
2. Kupokea rushwa pindi wanapo pewa na kuomba waongezewe zaidi.
Magari ya kusafirisha abiria huwa abiria wanashuhudia ila watu huwaza wafike tu salama na kwa wakati katika safari zao lakini huwa ni kitendo kinacho kera abiria, japo madereva huwa na msemo kuwa "mkono mtupu haulabwi" ila ukweli ni kuwa wanakereka pia.
Utu ni muhimu kuliko pesa na usalama wa taifa ni jukumu la vyombo vya usalama(jeshi la polisi).