Ili kuendeleza shughuli za kimaendeleo Tanzania, serikali ya Tanzania imekopa kutoka nje. BOT July 2019 ilisema deni la nje limefikia Dola Billion 21.6 sawa na Trillion 49Tsh na deni la ndani ni Trillion 15.5Tsh.
Kufikia January 2020 deni la nje limekuwa mpaka kufikia Trillion 54Tsh.
Janga la Corona limesababisha maafa katika nchi nyingi hasa kupunguzua kasi ya ukuwaji wa uchumi katika nchi nyingi, jambo ambalo limefanya Tanzania kukopa pesa na kupokea misaada mbali mbali kutoka nchi za nje,
Mikopo na misaada Tanzania iliyopokea kwanzia Jangala Corona kuanza ni kama ifuatavyo.
1. Tanzania ilipokea euros million 27 kutoka EU ili kusaidia katika kupambana na janga la corona.
2. June 2020 Tanzania ilipokea hazina na misaada ambayo inathamani ya Dola million 14.3 kutoka International Monetary Fund.
3. September 2020 Tanzania ilikopa US Dola million 3.79 kutoka Worl Bank ili kusaidia katika matumiza ya maabara ya Taifa katika ugunduzi wa COVID-19 cases.
4. October 2020 Tanzania ilikopa Dola million 50.7 kutoka African Development Bank kwaajili ya kupambana dhidi ya corona.
5. Vile vile Tanzania ilipokea Dola million 500 kutoka World Bank kwaajili ya elimu ya kisasa.
6. Tanzania imeomba mkopo wa dola million 11 kutoka Global Fund(japo haiko wazi kama mkopo ulikubaliwa au la).
Sasa swali la kujiuliza ni kwamba, kama Siku tatu za maombi iliondoa Corona Tanzania pesa ambazo Tanzania iliokea September na October zilikuwa za nini na zilifanya shughuli gani wakati Corona ilishakwisha?
Mikopo ambayo Tanzania imepata kutoka nje inazidi kuongeza deni la nje, je serikali yetu ina jambo gani la kusema kuhusu hili.
Je bado deni la nje Tanzania inaweza kulimudu?
Je kodi za wananchi zinatumikaje mpaka kuwe na madeni makubwa namna hii?