Katika maisha kuna vitu vingi sana ambavyo vinamfanya mtu asiwe na maendeleo anayoyahitaji na huwenda akawa anawaza kubadilika au anasema nataka kubadilika.
UKIHITAJI MABADILIKO KATIKA MAISHA YAKO UNAWEZA BADILI VITU KADHAA KATIKA MAISHA YAKO ILI UONE MAFANIKIO.
1. Amuzi la kubadilika litoke moyon mwako likisapotiwa na akili yako, nimesema hivyo kwa maana ya kwamba mtu anaweza sema nataka kubadilika manenl ambayo ameyatoa tu moyon mwake ila ukwel ni kwamba amesema tu ili awape wenzake mada ya kuongelea ila sio kama ameamua kutoka moyon mwake mwishowe anajikuta anaendelea kama vile alivyokuwa au alivyo sasa.
2. Badili fikra/mawazo yako, hapa ndo pale unaambiwa fikiri nje ya box, yaan kama ulikuwa unapata pesa alafu wazitumia kwa starehe fanya upunguze starehe na ufanye jambo la maendeleo zaidi au fikiri ni jinsi gan utakuza kipato chako zaid mpaka ufikie malengo yako katika maisha yako.
3. Badili aina ya maisha unayoishi/life style, kama ulikuwa mtu wa starehe sana punguza au acha kama ulikuwa unakaa tu anza kwa kufanya kazi, kama ulikuwa wqmtegemea mtu anza kujitegemea mwenyewe.
4. Plan maisha yako, uwe na mipango na malengo katika maisha yako uwe na mpango wa mda mfupi na mipango ya mda mrefu na mipango hiyo sio unaipanga tu na kuitekeleza pia mfano baada ya miaka mitano unajiona umefikia wapi katika maisha yako??
5. Baki na marafiki ambao wanafaida kwako, marafiki ni asset na kuna asset za aina tatu, kuna asset ambazo hiwa hazina faida, asset ambazo hujaza tu nafasi na hazina faida na kuna asset ambazo zinafaida kwako sasa hawa wenye faida ndo wa kwenda nao sambamba maana watakupa challenge nyingi katika maisha na ikitokea siku umekwama wanaweza kukusaidia.
6. Mavazi yako/dressing code, sio lazima kubadili mavaz yako ila angalia mavazi uliokuwa unavaa yanakuletea heshima au la kama hayakuletei heshima anza kuvaa mavazi yatakayo kuheshimisha mbele za watu.
7. Usisikilize walimwengu sana, binadamu huwa hatukosi cha kusema maana mtu akifanya na asipo fanya pia tutasema tu maana hatukosagi cha kusema. Kamwe hutaweza kumfurahisha mlimwengu hata ufanye kitu gan ambacho amekutaka ufanye cha msingi jifurahishe wewe mwenyewe tu na watakao kuwa karibu nawe watafurahi na wewe.
8. Uthubutu, nimesema hivi kwa maana kuwa watu wengine wanajiuliza ntaanzaje kubadilika mimi ila ukiwa na uthubutu ni lazima utabadilika ila kama huna utakata tamaa na kubaki kama zaman.
9. Tekeleza mipango yako, unaweza ukawa na wazo au jambo lakini bila kulitekeleza utabaki pale pale alafu utaanza kujiuliza kimetokea nini ila tatizo lipo kwa wewe mwenyewe maana umeshindwa kutekeleza jambo lako mwenyewe, usisubiri kutekelezewa na mtu ni muhimu kutekeleza mwenyewe ili ujue ugumu na urahisi wake. Pia utakuwa unajua uchungu wa kukipoteza ulicho kitekeleza.
Safari ya mabadiliko katika maisha inamilima na mabonde mengi sana, kuna muda utakata tamaa lakini angalia ni wapi unataka kuwepo, ni wapi unataka kufika na ni wapi unataka maisha yako yafikie, yale mafanikio ndio malipo yako wewe kwaiyo pambana mpaka ufanikiwe katika maisha na utimize malengo yako.