Thursday, 4 July 2019

MABADILIKO YANAANZA NA WEWE (CHANGES BEGINS WITH YOU)

Ukitaka mabadiliko yawepo Tanzania  ni lazima Watanzania tubadilike kwanza,tubadili frika zetu, tukubali kubadili mifumo yetu yote kikubwa zaidi tukubaliane na mabadiliko. Mfano mzuri United States Of America mfumo wao wa SIASA uko vizuri sana na wananchi wao wanapenda mapadiliko, Raisi alieko madarakani kama hajatimiza sera zake zote alizo ahidi kipindi cha kampeni wanampiga chini wanampa mtu mwingine uongozi tena baada ya miaka minne tu bila kujali kiongozi wao anatoka kwenye chama gain ila wanaangalia liongozi huyo anasera zipi, na kama hizo sera zinataleta mabadiliko zaidi kwenye nchi yao. Lakini Tanzania mnampa mtu madaraka baada ya miaka mitano hajatimiza ata sera mbili alizo ahidi lakini baada ya miaka mitano mnamchagua mtu yuleyule na anakuja na sera zingine wakati zile za mwanzo hajatimiza na bado mnampa tena kura zetu sijui mnategemea kupata badiliko lipi wakati alishindwa kubadili nchi ndani ya miaka mitano aliyokuwa nayo, sasa anakuwa kiongozi kwa miaka kumi Tanzania inakuwa ile ile tuliyozoea tena mbaya zaidi inazidi kuwa masikini.
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana kwa kuwa na rasilimali asili kama gesi, makaa ya mawe, madini, vivutio vya wanyama etc  pamoja na kuwa na vitu vyote hivi Tanzania inazidi kuwa masikini ukilinganisha na Rwanda in nchi ndogo lakini ni tajiri kuliko Tanzania.
Kenya ilipata uhuru baada ya Tanzania lakini kiuchumi tunawasikilizia mbali kinyama # Tanzia tunafeli wapi is it ignorance that we ca not use our our natural resource to save our country and its people or is it that poverty has higher affinity to Tanzania?.
Tanzanite ni madini yanayopatikana Tanzania tu ndio maana yanaitwa Tanzanite lakini kwenye soko la dunia nchi ya kwanza inayojulikana kwa kuuza Tanzanite ni South Africa ikifatwa na Kenya, Watanzania tunafeli wapi

Thursday, 30 May 2019

NAFASI YA UTHUBUTU KWA VIJANA( YOUTH DARE TAKING CHANCES AND RISKS)

Kwa soko la ajira lilivyo Tanzania ni wakati wa vijana kuamua kuthubutu kufanya mabotofauti tofauti ya kuichumi badala ya kubaki na kulalamika kuwa ajira hamna, ni wakati wako kijana kujiongeza na kuacha kuota ndoto na kuamka na kuifanya ndoto yako kuwa kweli, unaweza kuwa na ndoto ya kuwa;
1: mwanasiasa ni wakati wako kuonyesha mabadiliko kama damu changa na kuleta maendeleo kwa jamii inayokuzunguka nakuwa legend.
2: mfanya biashara na mwishowe kuwa na kampuni yako na kuajiri watu ambao bado wanasubiri kuajiriwa wakati wewe uliamua kuthubutu na kubadilisha maisha yako.
3:kuwa mkulima. jambo ambalo vijana wengi hawalipendi lakini ukweli kilimo kinapesa kuliko ata ukiwa na ajira nakupata mashahara.
4:mtangazaji, onyesha juhudi zako katika kazi zako huwenda itafika wakati ukaanza na stesheni moja tu lakini mwisho wa siku ukapata kampuni yako na kuajiri vijana wengi katika kampuni yako.
5:KIJANA UNAWEZA KUWA MTU YOYOTE NA KWA WAKATI UTAKAO NI WEWE TU KUAMUA KUFANYA MABADILIKO KATIKA FIKRA ZAKO NA KUONA KWAMBA KILA JAMBO LINAWEZEKANA KATIKA MAISHA YAKO.
Kila tajiri aliyeko apa duniani hakuzaliwa tajiri ila alitafuta na alithubutu ndio maana amefanikiwa
Power of positivity and daring is the perfect combination to success, when you want to have a better tomorrow you must have a planned today.

Tuesday, 5 March 2019

SI LAZIMA KIONGOZI BORA KUTOKA KATIKA CHAMA KIMOJA KILA BAADA YA MIAKA MITANO

Imagine wanasiasa wangapi apa nchini wametimiza ahadi zao ambazo walikuwa wanazitoa wakat wa kampeni zao au nikwamba walikuwa wanatafuta kupata kura za wanannchi ili wapate nafasi ya kuingia bungeni bila kuleta mabadiliko yale waliokuwa wanaahid wanannchi wao, ni wakat wa kujiuliza kuwa wale ambao mmewapatia kura zenu wakati wa uchaguzi awamu hii mpaka sasa wameshakamilisha ahadi ngapi katika maeneo waliyotokea au kwa wanannchi anao wawakilisha, huduma za kijamii zimeboreshwa au zina zidi kuzorota maana mda unavyozidi kwenda nachokiona ni kwamba wananchi wanazidi kutoa kodi tu wakati ukienda hospitali tena hasahasa za wilaya unaambiwa hamna dawa sasa kodi za wanannchi zinafanya kaz gani kuwasaidia wanannchi?
Kuna sehem zingine mpaka sasa hakuna kilicho badilika kinachoonekana zaidi ya jengo la halmashauri kuzidi kupauka/ becoming older hata kupaka rangi tu wameshindwa, unafikiri watakuwa na uwezo wa kusaidia watu wake alafu cha kushangaza mmbunge wao yupo tu halioni hilo na haoni kama hajaleta badiliko kwa eneo alilotoka alafu akifika bungeni chamaana anachokifanya na kinaonekana kwa kweli ni kulala tu au kuongea mambo ambayo sio muhimu, unakutana na mbunge utadhani si kiongozi kabisa.
I think ni wakati wa wanannchi kuamka na kujaribu mambo mapya ili kupata wanacho hitaji kuliko kwenda kimazoea na kuzidi kupoteza vitu walivyonavyo, try new things for better results rather than not taking the risk and regreat later, mfano sio lazima kuchagua kiongozi kutoka chama cha CCM sababu ndio chama kinachoshindaga jaribu kuchagua kiongozi  bora hata kama si wa CCM,mda mwingine watu hufanya vitu kwa mazoea ila mkionyesha kwamba mnahitaji viongoz bora bla kujali anatokea kwenye chama gani itasaidia sana kuwapa changamoto wanasiasa wote maana hakuna atakae kuwa amajua kama awamu ijayo atachaguliwa nani, wanatakiwa watimize ahadi zao na sio kukaa tu kwa miaka mitano madarakan bila kufanya chochote cha maana  mfano kuna sehemu moja hivi kunakuwaga na mto (Mto Magara) in aunganisha arusha na manyara, wakati wa mvua huwa hapapitiki sasa kila kiongozi atakwambia kuwa mkinipatia kura zenu nitahakikisha daraja linajengwa lakini sikilizia baada ya miaka mitano tena ilo swala linakuwa swagga tena.
Kiongozi akiongoza kwa miaka mitano na hajafanya chochote cha maana hiyo miaka inamtosha kabisa chamsingi ni kumpatia mtu mwingine miaka mitano kuona jipya lipi atafanya ndani ya miaka mitano ijayo. Kuweni makini sana kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi.
Si lazima kiongozi kutoka katika chama kimoja kila baada ya miaka mitano kama kweli mtakuwa mnataka kuchagua kiongozi bora na si kwa mazoea ya kuchagua chama maana ukweli ni kwamba wananchi wengi huwa wanachagua chama na si kiongozi.
Watanzania mkitaka mabadiliko ni wakati wa kuanza kuchagua viongozi na si chama bila kujali kabila.