Tuesday, 5 March 2019

SI LAZIMA KIONGOZI BORA KUTOKA KATIKA CHAMA KIMOJA KILA BAADA YA MIAKA MITANO

Imagine wanasiasa wangapi apa nchini wametimiza ahadi zao ambazo walikuwa wanazitoa wakat wa kampeni zao au nikwamba walikuwa wanatafuta kupata kura za wanannchi ili wapate nafasi ya kuingia bungeni bila kuleta mabadiliko yale waliokuwa wanaahid wanannchi wao, ni wakat wa kujiuliza kuwa wale ambao mmewapatia kura zenu wakati wa uchaguzi awamu hii mpaka sasa wameshakamilisha ahadi ngapi katika maeneo waliyotokea au kwa wanannchi anao wawakilisha, huduma za kijamii zimeboreshwa au zina zidi kuzorota maana mda unavyozidi kwenda nachokiona ni kwamba wananchi wanazidi kutoa kodi tu wakati ukienda hospitali tena hasahasa za wilaya unaambiwa hamna dawa sasa kodi za wanannchi zinafanya kaz gani kuwasaidia wanannchi?
Kuna sehem zingine mpaka sasa hakuna kilicho badilika kinachoonekana zaidi ya jengo la halmashauri kuzidi kupauka/ becoming older hata kupaka rangi tu wameshindwa, unafikiri watakuwa na uwezo wa kusaidia watu wake alafu cha kushangaza mmbunge wao yupo tu halioni hilo na haoni kama hajaleta badiliko kwa eneo alilotoka alafu akifika bungeni chamaana anachokifanya na kinaonekana kwa kweli ni kulala tu au kuongea mambo ambayo sio muhimu, unakutana na mbunge utadhani si kiongozi kabisa.
I think ni wakati wa wanannchi kuamka na kujaribu mambo mapya ili kupata wanacho hitaji kuliko kwenda kimazoea na kuzidi kupoteza vitu walivyonavyo, try new things for better results rather than not taking the risk and regreat later, mfano sio lazima kuchagua kiongozi kutoka chama cha CCM sababu ndio chama kinachoshindaga jaribu kuchagua kiongozi  bora hata kama si wa CCM,mda mwingine watu hufanya vitu kwa mazoea ila mkionyesha kwamba mnahitaji viongoz bora bla kujali anatokea kwenye chama gani itasaidia sana kuwapa changamoto wanasiasa wote maana hakuna atakae kuwa amajua kama awamu ijayo atachaguliwa nani, wanatakiwa watimize ahadi zao na sio kukaa tu kwa miaka mitano madarakan bila kufanya chochote cha maana  mfano kuna sehemu moja hivi kunakuwaga na mto (Mto Magara) in aunganisha arusha na manyara, wakati wa mvua huwa hapapitiki sasa kila kiongozi atakwambia kuwa mkinipatia kura zenu nitahakikisha daraja linajengwa lakini sikilizia baada ya miaka mitano tena ilo swala linakuwa swagga tena.
Kiongozi akiongoza kwa miaka mitano na hajafanya chochote cha maana hiyo miaka inamtosha kabisa chamsingi ni kumpatia mtu mwingine miaka mitano kuona jipya lipi atafanya ndani ya miaka mitano ijayo. Kuweni makini sana kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi.
Si lazima kiongozi kutoka katika chama kimoja kila baada ya miaka mitano kama kweli mtakuwa mnataka kuchagua kiongozi bora na si kwa mazoea ya kuchagua chama maana ukweli ni kwamba wananchi wengi huwa wanachagua chama na si kiongozi.
Watanzania mkitaka mabadiliko ni wakati wa kuanza kuchagua viongozi na si chama bila kujali kabila.




No comments:

Post a Comment