Wasomi wengi sana especially ambao bado wapo mashuleni huwa wanafikiria kuwa watasoma mpaka shule ya msingi,sekondari,sekondari ya juu na chuo baada ya chuo wataajiriawa nakufanya kazi na kupokea mshahara alafu watajenga nyumba na kuwa na maisha mazuri.
- Mfumo wa elimu Tanzania unaanda wasomi waje kuwa waajiriwa na sio kujiajiri mwenyewe wala kujitegemea kwa kipato.
Sasa maisha baada ya chuo kwa wasomi wote huwa yanakuwa hivi
- Kuna wale ambao watakuwa wanajitolea na hawalipwi kabisa
- Kunaambao watakuwa wanajitolea na kulipwa kidogo, inafika wakati wanaona mda unakwenda na hakuna connection zozote zile mwishowe wanaacha
- Kuna ambao watakwenda kufanya biashara mtaani(best of all)
- Kuna ambao watakuw wapo nyumbani tu hawana hili wala lile wanaangalia degree zao na kuchagua kazi maana wanaona hawana hadhi ya kufanya kazi ambazo sio za kisomi(worst kind)
- Kuna ambao watapata ajira katika sekta binafsi lakini wanaona kipato hakikidhi mahitaji
- Kuna ambao watakuja kuwa wadangaji kwasababu ya ugumu wa maisha
- Kuna ambao watakuwa wanapiga mishe za hapa na pale ili kupata hela za kuishi(mishen town)
- Kuna ambao watakuwa wakulima
- Kuna ambao watakuwa wafugaji
- Kuna ambao watakuwa inspiration talkers reality they got nothing
- Kuna ambao watakuwa wanabeti tu na kukwambia ramani hazisomi
- Kuna ambao watakwenda kusoma masters
- Kuna ambao watakuwa wanasiasa tu kwasababu wanatafuta pakutokea
- Kuna ambao wataamua kuwekeza kwenye haya makampuni kama global alliance, forever living c, oriflame, na mengineyo mengi mpaka waje kusanuka kuwa huo mfumo hauwafaidishi wao ila walio tangulia kabla ndio wanaopata faida
- Kunaambao watakuwa wanajaribu kupata mafanikio the hard way(strugglers) ambao siku zote huwa watafanikiwa
- Kunaambao watakuwa wanajaribu hili na lile lakini huwa wanakata tamaa mapema na kushindwa kufikia lengo.
- Huwa kuna aina nying sana za maisha na watu ambao watatokea baada ya masomo na baada ya kuanza maisha ya uraiani.
- News flash kwa wasomi wote kwamba the struggle is real especially to those ambao mnasoma bado muwe na mind set kwamba nikimaliza masomo sio lazima niajiriwe buni mbinj za kujipatia kipato ili uweze kuwa na maisha mazuri huko mbeleni, uwe umesoma ama haujasoma biashara au kazi yeyote ile hufanywa na watu wote hainaga kiwango cha elimu sema tofauti utaionyesha wewe ambae umesoma kwa kuifanya kazi yako kisomo na kwa uweledi wa juu kabisa onyesha elimu yako inakusaidi vipi kufanya biashara ama kazi uliyochagua kuifanya kwa quality ya juu kiasi gani ili iwe tofauti na ya watu wengine.
- Think critically kama kwel wataka kutoka kimaisha jiwekee goals au target ya kwamba baada ya mwaka au miaka mingapi wataka kuwa na mafanikio kiasi gani, wataka kuwa na maisha ya aina gani ila sio kulala na kuwaza hela mwishowe uje kupata depression bure wakati haujishughulishi
- Kuwa na role model ambae utakuwa unalook up to him and desire to be economically better than him or at least reach where he is and more.
Siku zote huwa nasema if you want to be remembered with the future generations leave the greatest legacy behind you will never be forgotten.
BE THE LEGEND.