Saturday, 5 August 2023

KUTUMIA PESA NDOGO KIJIPATIA KIPATO

​Ujasiriamali; leo Tuendelee na ile maana nyepesi ya ujasiriamali ni kuwa na shilingi elfu kumi na kuizalisha ikupatie shilingi elfu 15 au 20.

 Ukiwa na mawazo chanya ya kuwa utafanikiwa kaitika kutafuta kwako basi mafaniki yako lazima utayaona tu



TABIA ZA MJASIRIAMALI

​Ujasiriamali, kwa maana nyepesi tu ni kujipatia kipato kupitia shughuli mbali mbali ambazo mtu anazifanya ili kujiinua kiuchumu au kukuza uchumi wake.

Ujasiriamali unahusiasha au unaambatana na shughuli mbali mbali ambazo kwa watu wengine wanaweza wakaziona hazina faida sana au sio za msingi sana lakini mwishoni ikawa inafaida kubwa sana.

Kuna wajasiriamali wa viwango tofauti tofauti; 

Wajasiriamali wakubwa; hawa ni wale ambao biashara zao tayar zimeshakuwa na mtaji wao uko stable tayar na pia wanauwezo wa kuwaajiri watu mbali mbali katika kuimarisha shughuli zao

Wajasiriamali wa kati; hawa ni wale ambao wameshazoea biashara zao na wanajua changamoto zake na wanajua vipi watatatua changamoto hizo na soko pia linaenda vipi na wateja wanauhitaji wa bidhaa zipi

Wajasiriamali wadogo wadogo; watu weng wapo hapa na wanahitaji elimu zaidi ili kufahamu changamoto nyingi ambazo zipo na vip watatatua na soko linahitaji nini zaidi pia mtaji unaweza ukawa sio mkubwa sana na kwenye kiwango hichi mtu akifanya uzembe biashara yake hufa kabisa 


 Sasa leo nataka niwape fact  kuhusu ujasiriamali, tufahamu tabia za wajasiriamali zinakuwa vipi?

1. Mchapakazi; namaanisha kufanya kazi kweli kweli na kihodari anafanya shughuli zake kutokana na msukumo anaoupata kutoka ndani mwake ili apate bidhaa bora na zenye kiwango ili apate wateja na awe na soko la bidhaa zake.

2.Kujiamini; mjasiriamali lazima ajiamini kutokana na vile vitu ambavyo anavifanya kama huduma katika jamii na aone umuhimu wake na pia akijiamini hawezi kukatishwa tamaa na watu wanaomzunguka mpaka atimize lengo lake

3. Mbunifu; mjasiriamali lazima awe mbunifu ili angalangu aweze kuendana na mahitaji ya soko na pia kukuza kipato chake na uchumi wake

4. Kuwa na lengo; mfano umeanza na mtaji wa elfu kumi unajiwekea lengo mpaka kufika  miezi kadhaa au baada ya mwaka unataka uwe umekuza mtaji kufikia kiasi kadhaa kwaiyo lengo lako litakupa msukumo wa kupambana zaid na zaidi

5. Matumizi ya rasilimali mbalimbali ambazo zinamzunguka; point kubwa ya ujasiriamali ni ubunifu na kujitahid kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa pesa kidogo zenye quality za hali ya juu, kama mjasiriamali anauwezo wa kutumia vitu mbalimbali vinavyomzunguka kuongeza thamani kwenye hivyo vitu na kupata faida zaid ni jambo zuri sana.

6. Uwezo wa kujifunza kutoka kwa wengine; kuwa na uwezo wa kujifunza kutoka kwa wengine ili angalau usijefanya makosa yale yale ambao wengine waliyafanya yakawarudisha nyuma katika shughuli zao pia kushiriki katika makongamano tofauti tofauti ili kuongeza zaid na zaidi elimu ya ujasiriamali ambayo unayo.

7. Kuwa na mawazo chanya; katika kila changamoto unayopitia, uwe mtu ambae unaweza kuamini kuwa leo hali ni mbaya ila kuna kesho na kesho itakuwa nzuri kuliko leo sio tatizo dogo tu tayar limeshakukatisha tamaa ila ukiwa na mawazo chanya itakusaidia kuendelea kupambania jambo zako zaid na zaidi.

8. Mwaminifu; katika jambo lolote ambalo unalifanya ukiwa mwaminifu basi  jambo lako litafanikiwa kwasababu watu wengine watakuja kwako kwasababu wanajua wewe ni muaminifu na kila jambo unalifanya kikamilifu.

9. Kutamani mafanikio; hakuna mjasiriamali ambae anafanya jambo ili lisifanikiwe anakuwa anapenda mafanikio sio yake tu bali hata na ya wengine ili apate cha again zaid na apate kuwa mbunifu zaid na zaidi.

10. Pesa kama kipimo cha mafanikio; nasema pesa sababu hakuna mtu anaefanya kazi ili asipate pesa kwaiyo mwisho wa siku unaangalia kama kabla na baada ya kuwa mjasiriamali pesa zako zimeongezea vipi utajua tu kuwa umefanikiwa au la.


Katika kipindi hiki cha sasa ambacho soko la ajira limekuwa gumu ni vizur zaidi kujiongeza angalau usije ukajikuta unaishi maisha ya taabu na njia nzur zaidi ya kujipatia kipato ni kufanya kazi na kujikuza kiuchumi kwa sasa na baadae pia.

CHUMA JUANI UKIWA KIJANA ILI UJILIE VYAKO KIVULINI UKIWA MZEE

Tuesday, 28 March 2023

*MHE. KIKWETE AELEKEZA WARATIBU WA TASAF KATIKA HALMASHAURI KUPATIWA ELIMU YA KUWAHUDUMIA WALENGWA KWA UPENDO.*

Lengo la kuanzishwa kwa TASAF ni kuwawezesha watu wasiojiweza kabisa kiuchumi kuondokana na hali iyo duni kuwapa ruzuku itakayowasaidia kupiga hatua ya maendeleo kiuchumi, hivyo ni vyema waratibu wakapewa ujuzi ya namna ya kuwahudumia walengwa hao.


Mh Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Dar Es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa TASAF.


Mh Kikwete amesema "Lengo la kuanzishwa kwa TASAF ni kuwawezesha watu wasiojiweza kabisa kiuchumi kuondokana na hali iyo duni kuwapa ruzuku itakayowasaidia kupiga hatua ya maendeleo kiuchumi, hivyo ni vyema waratibu wakapewa ujuzi ya namna ya kuwahudumia walengwa hao".


Kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya waratibu wa TASAF katika Halmashauri kutowahudumia vizuri walengwa wa TASAF, ni vema wakapewa elimu ya kuweza kuzungumza na walengwa kwani fedha zimetengwa kwaajili yao, wasipohudumiwa kwa upendo itakua haina mana ya kuanzishwa kwa mfuko huo.


Mh Kikwete amesema "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt Samia Suluhu anatamani kuona wananchi wote wanainuka kiuchumi, hivyo walengwa wakihudumiwa kwa upendo na kuelekezwa namna ya kutumia ruzuku basi malengo ya Mh Rais yatakua yamefikiwa".


Aidha Mh Kikwete ameitaka Menejimenti hiyo kupitia kitengo cha habari kuuhabarisha umma juu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yao ioi kuepusha watu wasio na nia njema kuzungumza mabaya juu ya utekelezwaji wa majukumu ya TASAF.


Mh Kikwete amesema "TASAF inafanya kazi nzuri ya kuwainua walengwa kiuchumi, lakini mazuri hayo hayasemwi mara kwa mara, hivyo ni vizuri yakasemwa ili kuepukaba na watu wanaoharibu taswira nzuri ya taasisi na serikali kwa ujumla.

Saturday, 25 March 2023

HOW TO START A SUCCESSFUL BUSINESS THAT BRINGS PROFIT/ JINSI YA KUANZISHA BIASHARA INAYOINGIZA FAIDA.

Leo nataka niwaambie kitu kuhusu biashara, namaanisha jinsi ya kuifanya biashara yako ikuingizie faida na sio hasara , hapa ndipo mahali watu wengi hufeli. Sintakwambia sijui tengeneza mpango kazi fanya expected profit or loss / faida au hasara utakayo ipata kwa week au mwezi , Vitu muhimu vya kufahamu kwa wewe mfanya biashara au unategemea kuanzisha biashara yako.ndio mpango kazi ni mihimu tena muhimu sana ila kuna vitu vikikosekana hata kama unampango kazi mzuri basi biashara yako itafeli

Vitu muhimu vya kufahamu kwa wewe mfanya biashara au unategemea kuanzisha biashara yako.
1.commitment /kujitoa au kujitolea au kuwekeza muda wako katika kuijenga biashara yako, usipo weka muda wako katika biashara yako my friend iyo biashara itakufa kabla hujaianza.
2.kuthubutu usiogope kujaribu njia mpya za kukuza biashara yako jifunze kwa wale ambao tayar walisha kuwa wanafanya biashara na ujiongeze na usiogope kujaribu jambo jipya maana usipo jaribu hutaweza kujua kama kingefabya kazi au la.
3. Be innovative/ kuwa mbunifu katika biashara lazima uwe mbunifu sio sababu jiran yako anapika maandazi bas na ww upike maandazi swali ni je hayo maandazi yako yanautofauti gani na ya wengine yaani ni kitu gani kinakufanya uwe watofauti na kushawishi mteja arudi  na kesho tena??
4. Kauli, unaweza ukawa na vitu vizur lakini hupati mteja tatizo ni kauli yako unaweza ukawa na kauli chafu au huongei na wateja basi huwezi pata wateja mteja ndio bosi wako au mfalme wako kwaiyo akija mchangamkie mkaribishe kwa bashaha muulize ahitaji kitu gani mwonyeshe vitu tofauti tofauti mweleze na vitu vingine vilivyopo uone kama kesho hajarudi tena na atakuletea pia wateja wengine kutokana na kauli yako
5. Matumizi, usifanye matumizi au usitegemee biashara yako kwa kila kitu namaanisha unaanzisha biashara bado haijawa imara halafu unategemea pesa za matumizi yako binafsi kutoka kwenye biashara hiyo, biashara zote mwanzoni zinakula pesa badala ya kuingiza kwaiyo ukifanya kuitegemea kwa kila jambo biashara hiyo itafeli
6.kitahidi kuwa na miradi inayokuingizia pesa, usitegemee mradi mmoja ambao unakuingizia pesa  ndo ukawa kila kitu jiwekeze katika vitu tofauti tofauti uwe na vyanzo tofauti tofauti vya kukuingizia pesa hutojutia utakuja nishikuru baadae sababu kubwa ni kwamba kuna risk ambazo watu huwa hawazifikirii ambazo zinawezq kusababisha biashara yako ikapotea au kufa ukiwa na vyanzo vingi basi utaweza kujikimu vizur pia
7.management, sio kila mtu anaweza kaa katika biashara yake mwenyewe kwaiyo kama umeweka mtu basi hakikisha huyo mtu ni mwaminifu na anajua kufanya biashara namaanisha uwe umemchunguza mfanya kazi wako na kujua uwezo wake wa kikazi na umeridhika na kiwango chake cha kazi ndio umwache mwenyewe lakini pia hakikisha unakwenda kumtembelea katika biashara mara kwa mara ili kujua biashara inaendelea vipi.

Kama wahitaji kujua kuhusu mpango kazi/ business plan unaweza ukajifunza hili katika post yangu ambayo tayar nilisha itoa kwaiyo darsa huru unalipata hapa ukiwa na jambo la kuuliza usisiste  pia unaweza nipata kwa email happyissangya1@gmail.com na pia unaweza jiunga goup la whatsapp via https://chat.whatsapp.com/HVhM857PCIu4oemMIoAasu