Leo nataka niwaambie kitu kuhusu biashara, namaanisha jinsi ya kuifanya biashara yako ikuingizie faida na sio hasara , hapa ndipo mahali watu wengi hufeli. Sintakwambia sijui tengeneza mpango kazi fanya expected profit or loss / faida au hasara utakayo ipata kwa week au mwezi , Vitu muhimu vya kufahamu kwa wewe mfanya biashara au unategemea kuanzisha biashara yako.ndio mpango kazi ni mihimu tena muhimu sana ila kuna vitu vikikosekana hata kama unampango kazi mzuri basi biashara yako itafeli
every one is free to talk and make the country better, as long as the true democracy exists every one has a chance to contribute in changing the country either ur educated or not what matters more is what you say and if you can keep ur words.Freedom_free country_freedom of speech.
Saturday, 25 March 2023
HOW TO START A SUCCESSFUL BUSINESS THAT BRINGS PROFIT/ JINSI YA KUANZISHA BIASHARA INAYOINGIZA FAIDA.
Vitu muhimu vya kufahamu kwa wewe mfanya biashara au unategemea kuanzisha biashara yako.
1.commitment /kujitoa au kujitolea au kuwekeza muda wako katika kuijenga biashara yako, usipo weka muda wako katika biashara yako my friend iyo biashara itakufa kabla hujaianza.
2.kuthubutu usiogope kujaribu njia mpya za kukuza biashara yako jifunze kwa wale ambao tayar walisha kuwa wanafanya biashara na ujiongeze na usiogope kujaribu jambo jipya maana usipo jaribu hutaweza kujua kama kingefabya kazi au la.
3. Be innovative/ kuwa mbunifu katika biashara lazima uwe mbunifu sio sababu jiran yako anapika maandazi bas na ww upike maandazi swali ni je hayo maandazi yako yanautofauti gani na ya wengine yaani ni kitu gani kinakufanya uwe watofauti na kushawishi mteja arudi na kesho tena??
4. Kauli, unaweza ukawa na vitu vizur lakini hupati mteja tatizo ni kauli yako unaweza ukawa na kauli chafu au huongei na wateja basi huwezi pata wateja mteja ndio bosi wako au mfalme wako kwaiyo akija mchangamkie mkaribishe kwa bashaha muulize ahitaji kitu gani mwonyeshe vitu tofauti tofauti mweleze na vitu vingine vilivyopo uone kama kesho hajarudi tena na atakuletea pia wateja wengine kutokana na kauli yako
5. Matumizi, usifanye matumizi au usitegemee biashara yako kwa kila kitu namaanisha unaanzisha biashara bado haijawa imara halafu unategemea pesa za matumizi yako binafsi kutoka kwenye biashara hiyo, biashara zote mwanzoni zinakula pesa badala ya kuingiza kwaiyo ukifanya kuitegemea kwa kila jambo biashara hiyo itafeli
6.kitahidi kuwa na miradi inayokuingizia pesa, usitegemee mradi mmoja ambao unakuingizia pesa ndo ukawa kila kitu jiwekeze katika vitu tofauti tofauti uwe na vyanzo tofauti tofauti vya kukuingizia pesa hutojutia utakuja nishikuru baadae sababu kubwa ni kwamba kuna risk ambazo watu huwa hawazifikirii ambazo zinawezq kusababisha biashara yako ikapotea au kufa ukiwa na vyanzo vingi basi utaweza kujikimu vizur pia
7.management, sio kila mtu anaweza kaa katika biashara yake mwenyewe kwaiyo kama umeweka mtu basi hakikisha huyo mtu ni mwaminifu na anajua kufanya biashara namaanisha uwe umemchunguza mfanya kazi wako na kujua uwezo wake wa kikazi na umeridhika na kiwango chake cha kazi ndio umwache mwenyewe lakini pia hakikisha unakwenda kumtembelea katika biashara mara kwa mara ili kujua biashara inaendelea vipi.
Kama wahitaji kujua kuhusu mpango kazi/ business plan unaweza ukajifunza hili katika post yangu ambayo tayar nilisha itoa kwaiyo darsa huru unalipata hapa ukiwa na jambo la kuuliza usisiste pia unaweza nipata kwa email happyissangya1@gmail.com na pia unaweza jiunga goup la whatsapp via https://chat.whatsapp.com/HVhM857PCIu4oemMIoAasu
Labels:
Facebook,
google,
Instagram,
Printerest,
Tweeter.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment