Lengo la kuanzishwa kwa TASAF ni kuwawezesha watu wasiojiweza kabisa kiuchumi kuondokana na hali iyo duni kuwapa ruzuku itakayowasaidia kupiga hatua ya maendeleo kiuchumi, hivyo ni vyema waratibu wakapewa ujuzi ya namna ya kuwahudumia walengwa hao.
Mh Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Dar Es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa TASAF.
Mh Kikwete amesema "Lengo la kuanzishwa kwa TASAF ni kuwawezesha watu wasiojiweza kabisa kiuchumi kuondokana na hali iyo duni kuwapa ruzuku itakayowasaidia kupiga hatua ya maendeleo kiuchumi, hivyo ni vyema waratibu wakapewa ujuzi ya namna ya kuwahudumia walengwa hao".
Kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya waratibu wa TASAF katika Halmashauri kutowahudumia vizuri walengwa wa TASAF, ni vema wakapewa elimu ya kuweza kuzungumza na walengwa kwani fedha zimetengwa kwaajili yao, wasipohudumiwa kwa upendo itakua haina mana ya kuanzishwa kwa mfuko huo.
Mh Kikwete amesema "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt Samia Suluhu anatamani kuona wananchi wote wanainuka kiuchumi, hivyo walengwa wakihudumiwa kwa upendo na kuelekezwa namna ya kutumia ruzuku basi malengo ya Mh Rais yatakua yamefikiwa".
Aidha Mh Kikwete ameitaka Menejimenti hiyo kupitia kitengo cha habari kuuhabarisha umma juu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yao ioi kuepusha watu wasio na nia njema kuzungumza mabaya juu ya utekelezwaji wa majukumu ya TASAF.
Mh Kikwete amesema "TASAF inafanya kazi nzuri ya kuwainua walengwa kiuchumi, lakini mazuri hayo hayasemwi mara kwa mara, hivyo ni vizuri yakasemwa ili kuepukaba na watu wanaoharibu taswira nzuri ya taasisi na serikali kwa ujumla.