Mtaji wa masikini bwana ni nguvu zake kwaiyo anza na ulicho nacho embu fanya 2024 kuwa mwaka wa mabadiliko katika maisha yako.
Kwenye maisha tupo na hali tofauti za kiuchumi, kuna waliozaliwa wako na bahati kwao wako na pesa angalau anaweza kupewa mtaji ila ni vizuri kuwa na kile kitu unaweza sema kwa pride kwamba nichako na umekipambania mwenyewe.
Kuna ambao wao mtaji wao ni nguvu sasa panahitajika uvumilivu na mipango ili kupata kile unataka na kuwa na maisha ya aina fulani unayoyataka kuyaishi.
Nikisemema mataji wako ni nguvu zako na pia anza na kile ulichonacho namaanisha tengeneza plan/ mpangilio wa jambo unalotaka kulifanya na pia utengeneze picha kwenye akili yako kwenye miaka mitano ijayo unataka kuwa nani??
Mfano unafanya kazi unalipwa pesa ila sasa hakikisha kuna asilimia ya pesa hiyo unaiweka ili angalau jambo lako unalotaka kulikamilisha ulifanye.
Fact ni lazima kutumia pesa kutengeneza pesa ila kwenye matumizi ya pesa sasa ndio unaweza ukatumia pesa ndogo kuanzisha jambo lako na uzuri wa biashara ni kuwa biashara inakuwa kutokana na asilimia ya faida unakuwa unairudisha kwenye biashara yako.
Fact usitegemee kuona mafanikio kwa muda mfupi lazima kukuza jambo lako kwanza ndio utakapoona faida yake kwaiyo uvumilivu na ubunifu ni jambo la lazima.
Fact usitegemee kila hitaji lako katika jambo lako unalolifanya especially kama ni biashara utaishia kula mtaji wako.
Fact usiweke mayai yako yote katika kapu moja, jaribu kuwa na sehemu tofauti tofauti au biashara mbali mbali ambazo zinakuingizia maokoto
Fact simamia biashara zako mwenyewe angalau uwe na mtu mwaminifu na vile vile uwe unaonekana katika jambo lako angalau mara moja kwa siku kadhaa
Fact katika kila jambo fikiria vya mbeleni zaid usifikirie kesho tu maana kunakeshokutwa pia na namaanisha plan uwe nayo na muda mfupi na muda mrefu , plan ya muda mfupi itakusaidia kufanikisha plan yako ya muda mrefu.
No comments:
Post a Comment