Unaambiwa United Republic Of Tanzania ni democratic nations ila bhana hiyo demokrasia iko wapiii???
Wanasisa njoeni mnichape kama nimesema uwongo,
1. Ahadi zile zile ambazo hazitimizwi
2. Gharama ya maisha ndio inazidi kuwa ghali kila leo ila resources Tanzania inamiliki inatosha kwa Tanzania kuwa taji
3. Mikopo ya nje inazidi kuongezea ila project ambazo zinakamilishwa haziendani na fungu lililopekelewa kutoka pahali mmekopa.
4. Pesa ambazo zipo allocated kwaajili ya project fulani hazifiki kwa wakati katika maeneo husika na pia hakifiki kiasi halisi ambazo zilipangwa namaanisha hapo kati wamezipiga juu kwa juu.
5. Baada ya kupata kura hata kuongea na wananchi wako walio kupa fursa ili kuwasaidi hutaki ama ndo tuseme mnafunga tinted zenu.
6. Project nyingi ambazo zimekamilika zipo chini ya kiwango na mnafungia macho tu ila sababu mnaifahamu na watanzania wanafahamu pia ila kusema sasa ndio tatizo.
7. Kukosoa serikali ni kama jambo ambalo haliruhisiwi alafu bado mnasema eti Tanzania ni nchi huru.
8. Taasisi kama ya MAHAKAMA, TUME YA KUSIMAMIA UCHAGUZI na PCCB zipo chini ya serikali unategemea wanaweza kufanya kazi zao effectively bila kuwa waza mwajiri wake atamwondoa kazini bila kufikiria mara mbili.
Cha ajabu pahali panapoongoza kwa rushwa ni MAHAKAMA.
9. 2024 ni mwaka ambao vitu vingi vitafanywa kwa kulegezwa fulani ili kupata kura kirahisi.
10. 2024 ni mwaka ambao wasema ukweli wengi watapotezwa sana
Tukiwa wa kweli watanzania mnahongwa majiko madogo ya gesi, vitenge sijui khanga, tsheti na vielfu kumi hakafu unampa dhamana mtu ambae baadae anakuwa hana msaada kwako.
Natamani kucheka kama mazuri vile ila inasikitisha sana kama bado tutaendelea kufanya makosa yale yale kila baada ya miaka mitano kwa kujirudia rudia, najua ideology’s huwa zinatofautiana ila kutumia hata ule msemo wa MWAMBA NGOZI HUVUTIA KWAKE naona kama vile tunashindwa, wakati wa kuchagua usiangalie mtu anakupa nini kwa wakati ule ila angalia anauwezo wa kukupatia nini kwa baadae na kama kinafaida zaidi au la?.
DARASA HURU “UKIPEWA POKEA ILA AKILI KICHWANI KWAKO ANGALIA FAIDA YAKO YA BAADAE”.