Serikali ya Tanzania yaendelea kufanya mzaha kwa kutokuchukua hatua ambazo ni za hali ya juu katika kupambana na janga hili la corona virus.
Mpaka sasa hawajasitisha safari za ndege zinazotoka nje ya nchi wanaruhusu watu/watalii kutoka nchi zenye maambukizi kuingia nchini, haijakataza mikusanyiko kama makanisani,misikitini na cha zaidi sana wamefungua minada kifuatacho itakuwa ni kufungua shule na vyuo vyote.
Upimaji wa Corona virus hafifu yaani COVID-19 wao wanapima wasafiri tu ambao mpaka sasa wamefika 1.8m wakati Tanzania ina raia zaidi ya million 65, wanapima watu ambao waliokutana wa wagonjwa kama sio utani huo ni nini, mtu katokea airport amepanda usafir gani mpaka kwake amekutana na watu wa ngap kabla ya kufika kwake, kwa ujinga huu huu Tanzania itakuja kuwa na mlipo mkubwa sana katika siku zijazo maana tunachukulia janga hili kama utani tu.
Baadhi wa viongozi kupotosha watanzania eti Corona ni "mafua tu" Mr Makonda amesema ivo,, kwani nan ameshawahi kuona mafua yanaua Corona inauwa na huu ni mwanzo tu kama hatutajihadhari mapema tutakufa kama kumbikumbi tena na huduma zetu za Afya hizi zilizo zorota, tutakuja kuwekwa kwenye kitabu cha historia kwamba kulikuwaga na nchi moja inayoitwa Tanzania iliyoangamizwa na virusi vya Corona ikapotea kabisa katika uso wa dunia.
Kuwa na namba ndogo wa wagonjwa wa Corona ni kutokana na upimaji hafifu wagonjwa wa Corona jumla yafikia 22 lakini kama watanzania tujiulize ni kweli kuwa wapo 22? na je kati ya watanzania 65m wameshapimwa wangapi mpaka sasa?, maambukizi mapya ni watu wangapi? na je hatua ambazo zimechukuliwa dhidi ya kupambana na janga hili zinatosheleza?
Ni wakati watanzania tunatakiwa kupaza sauti zetu kusema kipi kifanyike, sisi ndio wapiga kuna na sisi ndio wenye mamlka na kumpa dola ambae yupo madarakani na yeye lazima atusikilize sisi,