Waathirika wa COVID-19 wapo 147 hawajasema kati ya watu wangapi waliopimwa wala juhudi gani zinaendelea ili kujua ni watu wangapi wamepimwa na maambukizi mapya yapo ngapi,vifo vitano na waliopona 11.
Shughuli zinaendelea kama kawaida maana watanzania lazima tufanye kazi ndio tupate kula lakini ni mbinu gani serikali inatumia kuwanusuru watu wake na janga hili?
Serikali mpaka sasa imeshapima wananchi wake wangapi?
Kuna maabara ngapi mpaka sasa zinapima COVID-19?
Kutokujali, kutokuogopa,kutokuwa na hofu ya janga hili ni jambo jema lakini itafikia wakati TANZANIA ITALIA NA ISIJUE WAPI PAKUANZIA NA WAPI PAKUISHIA.
No comments:
Post a Comment