jpm anafaa kwel 2020?Mtashangaa sana kwanini nasema kuwa 2015 uchaguzi ulifanyika na 2020 unafanyika tena.
Maana yangu kubwa ni kwamba utaona watu wengi sana wanasifia wanasiasa jambo ambalo sio baya ila watanzania tunatakiwa tuwaze sana ili tusije tukafanya mazoea kama tunavyofanya kila mwaka wa uchaguzi ukifika, hakuna sheria inayosema kwamba ni lazima kiongozi akae miaka kumi madarakani kama anafaa mpatieni dola aendeleze gurudumu lake la maendelea na kama hajatenda kama apaswavyo piga chini chagueni mwenye lengo jema la kuleta maendeleo.
1. Madiwani
..Jiulizeni sana diwani aliekuwepo madarakani amewatendea jambo gani la maendeleo katika kata zenu?
..diwani ametoa wazo gani katika kuleta maendeleo katika kata anayoitumikia?
..je diwani huyo mkimchagua tena atawaletea jambo gani katika kata yenu
Ni jukumu lenu kama wananchi kuchagua kiongozi bora ila mabadiliko na maendeleo ya patikane katika jamii yenu.
2. Wabunge
..mbunge wa wilaya yako amekuletea jambo gani la maendeleo kwa miaka mitano aliyokuwa madarakani?
Unfortunately mbunge wa wilaya niliyopo mimi yeye alichokifanya ndani ya miaka mitano ni kununua gari lake tu, hakai ofisini wala hoja zake zote alizotoa sidhani kama amezitimiza.
..je mbunge wako alitimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni miaka mitano iliyopita?
..je atafaa tena kuwepo madara kani?
3.Raisi
..raisi aliepo madarakani ametimiza hoja zake alizoto/ahidi wananchi?
..je ameleta maendeleo gani katika miaka mitano aliekuwepo madarakani?
.. Changamoto ya umasikini kwa mtu mmoja mmoja ameitatua vipi? Tena angalieni sana watu ambao wapo mijini na vijijini ambao wapo kwenye mzunguko wa umasikini usiangalie wale watu ambao ni matajiri ndio mtajua ninachokimaanisha ninauhakika kuna yule mtu apo mtaani kwako ambae unamuonea hafi huruma maana hata chakula cha siku hajui atakipataje na hajui hata kama kesho ataamka, anakula mlo mmoja siku nzima, nguo ndo bas tena kesho ikifika ni majaaliwa mateso yale yale ya jana tena bora na jana yake, masikini wamesaidika vip?
..Aliyotenda yanaonekana na ambayo hayajatendeka yanaonekana je ametenda kwa asilimia ngapi?
..kutokana na asilimia ulizo mpa je anafaa kuwa madarakani tena?
Watanzania tuko na tatizo moja tu yaan utazani tuanaugonjwa wa kusahau, msikubali kuhongwa vijihela vya mboga ya kula jioni tu alafu ukajitia hasara na kupoteza miaka mitano ambayo ungepata mafanikio na kupata pesa za kutumia miaka yote hiyo mitano na kwa siku nzima, tusikubali kuchagua mtu ambae hatatuletea badiliko lolote katika miaka mi tano ambayo unampa akaipoteza bure, tusikubali kugongwa kama mpira wa kona na kuingia nyavuni wakati ungekuwa unafutahia kuwa uwanjani unawapa wachezaji changamoto.
Tuondoe dhana kuwa kiongozi ni yule anaetoka chama fulani, hapana, kiongozi bora anatoka chama chochote, kiongozi mwenye sera na uchu wa maendeleo katika wilaya, kata, mtaa, na hata nchi yake huyo ndio kiongozi anaetufaa, kiongozi ambae anakuwa sauti ya kwel ya wananchi ndio anaefaa, kiongozi ambae akikaa hata katika familia yake anatamani na anakuja na wazo jipya ya kuiimarisha familia yake kiuchumi ndio anaefaa, kiongozi ambae anaona baada ya miaka mitano jamii yake ataibadilisha katika nyanja mbali mbali ndio anaefaa.
Mwaka wa uchaguzi tufanye maamuzi sahihi bila kushurutisha na nguvu ya vijihela vya chini ya kapeti wala nyuma ya pazia, tufanye maamuzi sahihi kwaajili ya baadae sio kwaajili ya sasa tu ata wajukuu zenu waje kuwakumbuka kwa kufanya jambo zuri huko baadae.
If you want to be a legend leave a great legacy behind no one will forget you forever.